148
Tunasimama Sayuni
Kwa uthabiti
1. Tunasimama Sayuni
Vijana shupavu,
Ahadi yatung’aria,
Wajibu ni wetu,
Msingi wa maadili
Kuuendeleza.
Twazimudu changamoto—
Wakweli daima!
2. Ukweli tufuatao
Wadharaulika.
Lakini tunapotii
Twajua twaweza
Kuyahimili maovu
Yaangamizayo.
Tunayo fimbo ya chuma,
Furaha ilimo.
3. Hofu na jaribu huja,
Ila hatuhofu.
Ni kwa ajili ya haki
Tunauthubutu.
Tutapenda, tutashinda;
Wimbo tutaimba
Kama vijana Sayuni—
Wasafi, imara.
Maandishi: Susan Evans McCloud, kuz. 1945. © 1985 IRI
Muziki: Lahani ya Ayalandi; mpangilio © 1985 IRI