Muziki
Mwokozi Ananipenda


188

Mwokozi Ananipenda

Kwa unyenyekevu

1. Hapo kale mahali pazuri,

Wana wakawa na Yesu.

Aliwafundisha kwa upendo.

Alitokwa machozi.

Na upendo ule kwa watoto

Hata kwangu upo.

Sijawahi kukaa na Yesu,

Lakini yu kweli kwangu.

[Chorus]

Anaishi!

Na nitamfuata.

Rafiki wa kweli,

Mwokozi ananipenda.

2. Nipo hapa mahali pazuri.

Nafunzwa kuhusu Yesu.

Wazazi watanisaidia

Njia iwe nyepesi.

Nimo kwenye mikono ya Yesu.

Nahisi upole.

Siku zote nitamfuata,

Nifike kwake mbinguni.

[Chorus]

Anaishi!

Na nitamfuata.

Rafiki wa kweli,

Mwokozi ananipenda.

Maandishi na muziki: Tami Jeppson Creamer, kuz. 1959, na Derena Bell, kuz. 1955

© 2002 na Tami Jeppson Creamer na Derena Bell. Haki zote zimehifadhiwa. Wimbo huu ni kwa matumizi ya kawaida, ya kanisa yasiyo ya kibiashara au matumizi ya nyumbani. Notisi hii lazima ionekane kwenye kila nakala iliyotolewa.