Muziki
Bwana Ni Nuru


41

Bwana Ni Nuru

Kwa uthabiti

1. Bwana ni nuru; ya nini hofu?

Wakati wote yupo karibu.

Ni wokovu wangu toka dhambini;

Na Roho hunipa ahadi hii.

[Chorus]

Bwana ni nuru;

Ni wimbo na furaha.

Siku, usiku,

Naongozwa daima.

2. Bwana ni nuru; hushinda giza.

Imani kuu, mbingu hupenya

Ambapo daima ni Mwenye enzi.

Hivyo kwa nini nibaki gizani?

[Chorus]

Bwana ni nuru;

Ni wimbo na furaha.

Siku, usiku,

Naongozwa daima.

3. Bwana ni nuru; ni nguvu yangu.

Kwa nguvu yake nitayamudu.

Mapungufu yangu huimarisha,

Kwa uaminifu nabarikiwa.

[Chorus]

Bwana ni nuru;

Ni wimbo na furaha.

Siku, usiku,

Naongozwa daima.

4. Bwana ni nuru, yote hakika.

Kwake hakuna giza kabisa.

Mkombozi wangu, Mfalme wangu.

Nitamsifu na watakatifu.

[Chorus]

Bwana ni nuru;

Ni wimbo na furaha.

Siku, usiku,

Naongozwa daima.

Maandishi: James Nicholson, 1828–1876

Muziki: John R. Sweney, 1837–1899

Zaburi 27:1

Isaya 12:2