Muziki
Njooni kwa Shangwe


114

Njooni kwa Shangwe

Kwa sifa

1. Njooni kwa shangwe,

Nyote mwaminio!

Njooni, mji mwema Bethlehemu.

O! Tazameni,

Bwana kazaliwa;

[Chorus]

Njooni tumwabudu;

Njooni tumwabudu;

Njooni tumwabudu,

Kristo, Bwana.

2. Imbeni kwa shangwe,

Enyi malaika;

Nyote mkaao juu mbinguni!

Sifa kwa Mungu,

Utukufu kwake!

[Chorus]

Njooni tumwabudu;

Njooni tumwabudu;

Njooni tumwabudu,

Kristo, Bwana.

3. Tunakusalimu,

Asubuhi njema;

Na utukufu wote uwe kwako.

Mwana wa Baba,

Sasa kazaliwa;

[Chorus]

Njooni tumwabudu;

Njooni tumwabudu;

Njooni tumwabudu,

Kristo, Bwana.

Maandishi: Yamehusishwa na John F. Wade, mnamo mwaka 1711–1786; Yametafsiriwa na Frederick Oakeley, 1802–1880

Muziki: Umehusishwa na John F. Wade

Luka 2:8–20

Zaburi 95:6