Muziki
Kwenye Siku ya Bwana


80

Kwenye Siku ya Bwana

Kwa kutafakari

1. Kumkumbuka Mwanao,

Tunakusanyika kwako

Kwa pamoja tunasali,

Na kujifunza injili.

Na kwenye siku ya Bwana,

Uwe nasi tunaomba.

2. Muda wote tukuwaze

Pia na wapendwa wote.

Kwa yote tuyafanyayo

Tusali bila kikomo.

Na kwenye siku ya Bwana,

Nyumbani kwetu kawia.

3. Tupate muda mzuri

Wa nguvu yako kuhisi,

Tutii sauti ndogo,

Tufanye mapenzi yako.

Na kwenye siku ya Bwana,

Nyoyoni mwetu bakia.

Maandishi: Paul L. Anderson, kuz. 1946

Muziki: Lynn R. Carson, kuz. 1942 © 1983 na Lynn R. Carson na Paul L. Anderson. Wimbo huu wa dini ni kwa matumizi ya kawaida, ya kanisa yasiyo ya kibiashara au matumizi ya nyumbani.

Moroni 6:5–6

Mosia 13:16–19