93
Kwa Unyenyekevu, Bwana
Kwa unyenyekevu
1. Kwa unyenyekevu, Bwana,
Twaomba Roho wako.
Twabariki sakramenti
Katika jina lako.
Mwokozi sitasahau
Ulivyo sulubiwa,
Ulivunjwa moyo wako
Juu ya msalaba.
2. Tuwezeshe kusamehe,
Tuwe wavumilivu.
Sala zetu zije kwako
Juu patakatifu.
Iwapo tutastahili,
Dhabihu takatifu,
Twakuomba tuwe nawe;
Tuwe na utukufu.
Maandishi: Mabel Jones Gabbott, 1910–2004. © 1948 IRI
Muziki: Rowland H. Prichard, 1811–1887