99
Tusifu Jina la Bwana
Kwa hamasa
1. Tusifu jina la Bwana,
Atukuzwe Yesu,
Aliyekufa Golgotha,
Kutuweka huru.
2. Aliyashinda mauti,
Kuleta wokovu,
Wenye dhambi kawaita,
Kuishi kwa Mungu.
3. Kashinda nguvu za kifo,
Kamshinda nyoka,
Amefungua kaburi,
Wafu kafufua.
4. Sakramenti ni ishara
Ya dhambi kuoshwa,
Shirikini na kukiri
Mnamkumbuka.
Maandishi: Richard Alldridge, 1815–1896
Muziki: Joseph Coslett, 1850–1910