96
Yavutia Kuuimba
Kwa unyenyekevu
1. Yavutia kuuimba
Upendo wake Muumba,
Alikuja—ni ajabu—
Kuokoa wanadamu.
[Chorus]
Kwani, Yesu alikufa,
Kuwakomboa wafungwa.
Hivyo hosana ziimbwe;
Nyote kiri upendowe.
2. Ni vyema kila Sabato,
Kama lilivyo agano,
Kuzikumbuka alama,
Imani kufanya upya.
[Chorus]
Kwani, Yesu alikufa,
Kuwakomboa wafungwa.
Hivyo hosana ziimbwe;
Nyote kiri upendowe.
3. O! Wasaa mtukufu!
Wote kuwa na walimu,
Kuadhimisha upendo
Na kuuenzi kwa nyimbo.
[Chorus]
Kwani, Yesu alikufa,
Kuwakomboa wafungwa.
Hivyo hosana ziimbwe;
Nyote kiri upendowe.
Maandishi: George Manwaring, 1854–1889
Muziki: Ebenezer Beesley, 1840–1906
Jina la tuni: HANCOCK
Mathayo 20:28