Muziki
Nisomapo Maandiko


159

Nisomapo Maandiko

Kwa sala

1. Nisomapo maandiko,

Baba wa wanadamu.

Nijaze moyo hekima,

Jaza fikira zangu.

2. Nisomapo maandiko,

Niguse roho, Bwana,

Nionyeshe maajabu

Kila ninaposoma.

3. Nisomapo maandiko,

Nionyeshe huruma.

Ufariji moyo wangu;

Niponye majeraha.

4. Nisomapo maandiko,

Nifikiri, nitii.

Neno lako ni uzima;

Nitembee nuruni.

Maandishi na muziki: C. Marianne Johnson Fisher, 1932–2018. © 1985 IRI

2 Timotheo 3:14–17

Warumi 15:4