98
Yesu, Mkombozi, Kristo, Bwana
Kwa sala
1. Yesu, Mkombozi,
Kristo, Bwana,
Hakika mauti,
Umeshinda.
Umetoka huko,
Kuja kwetu,
Na maisha yako
Ni dhabihu.
2. Na huu mkate,
Tunaula,
Twakuwaza wewe,
Kwa heshima.
Na yale mateso,
Pale juu
Ni upatanisho
Wa kudumu.
3. Tuyanywapo maji,
Taratibu,
Nyoyo hufurahi,
Na kusifu.
Tuongoze mpaka
Tuelewe,
Juu ya uzima
Wa milele.
Maandishi na muziki: Hugh W. Dougall, 1872–1963
Yohana 6:38–40
Yohana 15:13