Muziki
Malaika Waimba


120

Malaika Waimba

Kwa shauku

1. Malaika waimba

Utukufu kwa Bwana!

Amani duniani,

Kusamehewa dhambi!

Shangwe kwa mataifa;

Ushindi shangilia;

Tuimbe kwa vifijo

Amezaliwa Kristo

[Chorus]

Malaika waimba

Utukufu kwa Bwana!

2. Shangwe kwa Bwana Yesu!

Mwana Mtakatifu!

Kaleta na uhai,

Ukaja uponyaji.

Msalabani afa

Watu wasife tena;

Awafufue wote,

Pia awaokoe.

[Chorus]

Malaika waimba

Utukufu kwa Bwana!

Maandishi: Charles Wesley, 1707–1788

Muziki: Felix Mendelssohn, 1809–1847

Luka 2:8–14

3 Nefi 25:2