187
Bwana Mpendwa
Nyimbo ya Mwanavita wa Kidini
Kawaida, lakini kwa hisia
1. Nyota zang’ara
Na mbalamwezi,
Jua lawaka maradufu;
Yesu ang’ara,
Tena zaidi,
Anapenda kila mtu.
2. Mito mizuri
Nayo misitu,
Maua kote yamejaa;
Yesu mzuri,
Tena zaidi.
Hufanya nafsi kuimba.
3. Bwana mpendwa
Wa mataifa!
Mwana wa Adamu na Mungu!
Nitakusifu,
Na kuabudu,
Nitakusifu milele!
Milele!
Imba ubeti wa kwanza kwa sauti namna moja. Ubeti wa pili waweza kuimbwa kwa sauti namna mbili.
Maandishi: Hajulikani, karne ya 12
Muziki: Wimbo wenye asili ya Silesia; umepangiliwa na Darwin Wolford kuz. 1936. © 1989 IRI