Muziki
Nitamuiga Mwokozi


190

Nitamuiga Mwokozi

Kwa ujasiri

1. Nitamuiga Mwokozi

Na nitamfuata.

Nitapenda kama yeye,

Kwa ninayoyafanya.

Sichagui vyema kila wakati;

Najitahidi kuisikiliza sauti:

[Chorus]

“Pendaneni apendavyo Yesu.

Mwonyeshe huruma kila mtu.

Onyesha upole na uungwana;

Hivyo Yesu afundisha.”

2. Nitampenda jirani,

Nitamhudumia;

Nasubiri ile siku

Yesu ajapo tena.

Nikijikumbusha mafunzo yake,

Roho atanifundisha tena neno lake:

[Chorus]

“Pendaneni apendavyo Yesu.

Mwonyeshe huruma kila mtu.

Onyesha upole na uungwana;

Hivyo Yesu afundisha.”

Maandishi na muziki: Janice Kapp Perry, kuz. 1938

© 1980 na Janice Kapp Perry. Wimbo huu ni kwa matumizi ya kawaida, ya kanisa yasiyo ya kibiashara au matumizi ya nyumbani.