Muziki
Sikilizeni, Mataifa!


152

Sikilizeni, Mataifa!

Kwa ujasiri

1. Sikilizeni, mataifa!

Shangilieni kwa pamoja,

Malaika imbeni wimbo:

Nuru tena ipo!

[Chorus]

Injili, mwanga wa ukweli,

Wan’gara kutoka mbinguni,

Ni mng’aavu kama jua

Kote waangaza.

2. Watu walisaka gizani,

Wakakesha wakisubiri.

Sasa usiku umekwisha,

Nuru yarejeshwa!

[Chorus]

Injili, mwanga wa ukweli,

Wan’gara kutoka mbinguni,

Ni mng’aavu kama jua

Kote waangaza.

3. Tumeitwa na Mungu wetu ,

Kutumikia wote watu,

Tutasimamia ukweli,

Neno kuhubiri.

[Chorus]

Injili, mwanga wa ukweli,

Wan’gara kutoka mbinguni,

Ni mng’aavu kama jua

Kote waangaza.

Maandishi: Kutokana na maandishi ya Kijerumani na Louis F. Mönch, 1847–1916. © 1985 IRI

Muziki: George F. Root, 1820–1895

Mafundisho na Maagano 133:36–38

Mafundisho na Maagano 128:19–21