108
Ni Upendo Ulioje
Kwa utulivu
1. Ni upendo ulioje
Ulio kwa Baba
Kumtuma Yesu aje
Kuteswa na kufa!
2. Maishaye ya thamani
Kayatoa bure,
Japo hakuwa na dhambi,
Kuokoa wote.
3. Kwa utii akashinda
Zawadi tukufu:
“Kama utakavyo, Baba,”
Alisema Yesu.
4. Yesu alituonesha
Njia ya ukweli,
Kwenye mwanga na uzima
Kwa Mungu mbinguni.
5. Kukumbuka mwili wake
Mkate twakula,
Twaonesha kwa kikombe
Twamwamini Bwana.
6. Ni mkuu na kamili
Wokovu wa Bwana.
Rehema, pendo na haki
Vinaunganishwa.
Ubeti wa 1, 2, 5 na 6 unafaa zaidi kwa ajili ya sakramenti.
Maandishi: Eliza R. Snow, 1804–1887
Muziki: Thomas McIntyre, 1833–1914