Muziki
Bwana, Kwako Naja


125

Bwana, Kwako Naja

Kwa unyenyekevu

1. Ninakupenda, Mwokozi,

Napita njia yako.

Nitainua wengine,

Nipate nguvu kwako.

Ninakupenda, Mwokozi—

Bwana, kwako naja.

2. Mimi nani kuhukumu?

Nami siko kamili.

Mioyo kimya huficha

Masononeko mengi.

Mimi nani kuhukumu?

Bwana, kwako naja.

3. Nitawajali wengine,

Nijifunze kuponya.

Wahitaji na wanyonge,

Nitawahurumia.

Nitawajali wengine—

Bwana, kwako naja.

4. Nitapenda ndugu zangu

Jinsi unipendavyo.

Uwezo wako nipate

Nifanye kazi yako.

Nitapenda ndugu zangu—

Bwana, kwako naja.

Maandishi: Susan Evans McCloud, kuz. 1945. © 1985 IRI

Muziki: K. Newell Dayley, kuz. 1939. © 1985 IRI

Yohana 13:34–35

1 Yohana 3:16–19

1 Yohana 4:21