150
Nenda kwa Imani
Kwa shauku
1. Nenda kwa imani, taja
Yesu ndiye Kristo,
Na ndiye Mwana pekee;
Litangaze neno.
Nenda kwa matumaini
Injili eneza,
Kwamba wanadamu wote
Ni wana wa Baba.
2. Nenda kawaelezee
Udugu ni raha—
Kuwa twaweza kuishi
Milele pamoja.
Nenda uwahudumie,
Pasipo malipo;
Kisha utafurahia
Kazi yake Kristo
3. Nenda kwa nguvu useme
Kuna urejesho,
Tutaupata uzima
Kupitia Kristo.
Nenda hubiri ukweli,
Amani, furaha,
Ili watakaotii
Wamsifu Bwana.
Maandishi: Ruth M. Gardner, 1927–1999. © 1985 IRI
Muziki: Lyall J. Gardner, 1926–2012. © 1985 IRI
Mathayo 24:14