163
Ongokeni
Kwa uchangamfu
1. Ongokeni; Bwana aja,
Alisema Malaki.
Ongokeni kuandaa
Kazi iliyotukuka
Kwao wafu na hai.
2. Siku za mwisho Eliya
Ataleta agano.
Wote atawakumbusha
Ahadi zinazofunga
Watu tokea mwanzo.
3. Geuzeni nyoyo zenu
Kwao wale wazazi.
Watafute muwapate;
Hekaluni mkafungwe
Nao mwenu nyoyoni.
4. Geuzeni kwa watoto
Upendo wenu wote.
Matendoye ya injili,
Huduma za hekaluni,
Zibariki milele.
Maandishi: Paul L. Anderson, kuz. 1946. © 1983 Paul L. Anderson na Lynn R. Carson
Muziki: Gaylen Hatton, 1928–2008. © 1985 IRI Wimbo huu wa dini ni kwa matumizi ya kawaida, ya kanisa yasiyo ya kibiashara au matumizi ya nyumbani.