65
Baba Mbinguni
Kwa sala
1. Baba mbinguni, kwa upendo wako,
Utusikie pale tuombapo,
Twashukuru kwa amani milele,
Hata milele.
2. Mioyo ina amani ya Bwana,
Ni furaha kwa wakata tamaa.
Tuna imani na wewe milele,
Hata milele.
3. Mungu uyape mataifa nguvu,
Amani yako njia ya wokovu.
Hivyo tuweze kusogea mbele,
Tunyenyekee.
Maandishi: Angus S. Hibbard, 1860–1945
Muziki: Friedrich F. Flemming, 1778–1813; umepangiliwa na Edwin P. Parker, 1836–1925
Zaburi 29:11
Yohana 14:27