Muziki
Matendo Yako, Mungu wa Haki


151

Matendo Yako, Mungu wa Haki

Kwa sifa

1. Matendo yako,

Mungu wa haki,

Na njia zako

Ni za ukweli!

Nani haogopi

Jina la Mungu?

Hakuna mwingine

Mtakatifu.

2. Na wapotevu

Waangazie.

Ibada yao

Ikufikie.

Hukumu, ukweli,

Zitaenea,

Hadi watu wote

Wakiri Bwana.

Maandishi: Henry U. Onderdonk, 1789–1858; kulingana na Ufunuo 15:3–4

Muziki: Joseph Martin Kraus, 1756–1792

Ufunuo 15:3–4

Warumi 14:11