10
Neno Huleta Amani
Kwa kuabudu
1. Neno huleta amani
Kwao washirika.
Na mwangaza wa injili
Watuelekeza.
2. Maagizo ni ya Mungu
Anayetujali.
Upendowe mng’aavu
Kwao wafuasi.
3. Uongo humong’onyoka,
Nazo mila ovu.
Wingu lililotishia,
Lakiri u Mungu.
4. Heri tujualo Jina,
Tuziache dhambi.
Roho ataendelea
Kutuweka safi.
5. Punde shetani ashindwa
Na kuisha dhambi,
Shida hazitasumbua,
Wala kutuudhi.
6. Tulivyovipata nusu
Vitakamilika,
Kwani Bwana Mungu wetu
Atavirejesha.
7. Kwa subira twaziponya
Nafsi hadi aje.
Tuzidi kutumikia,
Ukombozi uje.
Maandishi: Mary Ann Morton, 1826–1897
Muziki: Alfred M. Durham, 1872–1957. © 1948 IRI
Zaburi 119:165
Zaburi 119:97–104