82
Mungu Awe Nanyi Daima
Kwa unyenyekevu
1. Mungu awe nanyi daima,
Kwa nasaha muongozwe,
Mbaki zizini mwake.
Mungu awe nanyi daima.
[Chorus]
Hadi tuonane tena,
Miguuni pa Bwana.
Hadi tuonane tena.
Mungu awe nanyi daima.
2. Mungu awe nanyi daima;
Shida zinapowazonga,
Awaoneshe huruma.
Mungu awe nanyi daima.
[Chorus]
Hadi tuonane tena,
Miguuni pa Bwana.
Hadi tuonane tena.
Mungu awe nanyi daima.
3. Mungu awe nanyi daima;
Nguvu ya upendo wake,
Imeshinda mambo yote.
Mungu awe nanyi daima.
[Chorus]
Hadi tuonane tena,
Miguuni pa Bwana.
Hadi tuonane tena.
Mungu awe nanyi daima.
Maandishi: Jeremiah E. Rankin, 1828–1904
Muziki: William G. Tomer, 1833–1896
2 Wathesalonike 3:16
Hesabu 6:24–26