73
Yesu Ninapokuwaza
Kwa unyenyekevu
1. Yesu ninapokuwaza
Nafurahi mno;
Na nitafurahi hasa
Nikikaa kwako.
2. Hakuna cha kukumbuka,
Wala jina tamu,
Jema na lenye baraka,
Kama lako Yesu!
3. Kwa wote wanyenyekevu,
Huwapa furaha,
Mkarimu kwa waovu
Wakikurudia!
4. Yesu, u furaha yetu,
U zawadi pia,
Ndiwe utukufu wetu,
Sasa na daima.
Maandishi: Yanahusishwa na Bernard wa Clairvaux, mnamo 1091–1153; yametafsiriwa na Edward Caswall, 1814–1878
Muziki: John B. Dykes, 1823–1876
Zaburi 104:34