101
Msalabani Golgotha
Kwa bidii
1. Msalabani Golgotha
Aliteswa Kristo,
Kifo kilikamilika
Kutakasa neno.
2. Kwa unyenyekevu kafa
Ili watambue,
Kifo hufungua njia
Ya mbingu milele.
3. Kifo cha Mwokozi wetu
Kilifanya upya
Ajabu ya ufufuo
Sote kuupata.
Maandishi: Vilate Raile, 1890–1954. © 1948 IRI
Muziki: Leroy J. Robertson, 1896–1971. © 1948 IRI
Luka 23:33, 46