134
Tuko Huru Kuchagua
Kwa dhati
1. Tuko huru kuchagua
Jinsi tutakavyokuwa;
Mungu hatulazimishi
Kurudi kwake mbinguni.
2. Aita, aelekeza,
Abariki kwa mwangaza,
Ni mkarimu, mzuri,
Na pia halazimishi.
3. Bila uhuru, busara,
Sisi ni kama wanyama,
Ambao hawafahamu
Peponi na jehanamu.
4. Tutumie mamlaka
Kuchagua yale mema;
Anafurahia Kristo
Tukitafuta upendo.
Maandishi: Hajulikani, mnamo 1805, Boston. Yalijumuishwa katika kitabu cha kwanza cha nyimbo za Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu ya Siku za Mwisho, 1835.
Muziki: Roger L. Miller, kuz. 1937. © 1985 IRI