Muziki
Acha Sayuni Ing’are


22

Acha Sayuni Ing’are

Kwa ujasiri

1. Acha Sayuni ing’are;

Nuruye yawaka.

Ajapo Mfalme wake,

Mbingu atagawa,

Kote lienee neno

Kuandaa watu

Kukutana na Henoko

Naye Bwana juu.

2. Parapanda pulizeni

Malaika wote.

Taarifa sambazeni

Duniani kote:

Kwamba Yesu kwenye mbingu,

Aja kuokoa

Walio Watakatifu,

Mwovu kuondoa.

3. Litaanza pumziko

Lililotangazwa,

Watakatifu na Kristo

Wataitawala

Milenia duniani;

Bwana, niandae

Nikae nawe Sayuni

Tusitenganishwe.

Maandishi: Edward Partridge, 1793–1840. Yalijumuishwa katika kitabu cha kwanza cha nyimbo za Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, 1835.

Muziki: Hajulikani, Württemberg, Germany, mnamo 1784

Mafundisho na Maagano 82:14

Musa 7:62–65