Muziki
Sauti ya Mwokozi


197

Sauti ya Mwokozi

Kwa utulivu

1. Ningelikuwa mtoto wakati wa Bwana,

Ningetembea naye na kumsikiliza.

Ila nisomapo neno napata amani.

Nahisi nasikia sauti ya Mwokozi.

2. Nabii asema yale Kristo angesema

Kama angekuwa hapa kuniongelesha.

Nabii anafundisha namna ya kuishi,

Nahisi naskia sauti ya Mwokozi.

3. Ninapofunzwa ukweli, namhisi Roho

Anifariji na kumshuhudia Kristo.

Anapoongea hujaza nafsi amani.

Nahisi nasikia sauti ya Mwokozi.

Maandishi na muziki: Sally DeFord, kuz. 1959

© 2007 na Sally DeFord. Haki zote zimehifadhiwa. Wimbo huu ni kwa matumizi ya kawaida, ya kanisa yasiyo ya kibiashara au matumizi ya nyumbani. Notisi hii lazima ionekane kwenye kila nakala iliyotolewa.