117
Usiku Mtulivu!
Kwa utulivu
1. Usiku mtulivu!
Ku kimya, ku ng’avu
Kote kwa mama na Mwana.
Mtukufu, Mwana mwanana,
Lala kwa amani
Lala kwa amani.
2. Usiku mtulivu!
Mchunga ahofu!
Utukufu watokea;
Mbingu yaimba Haleluya!
Azaliwa Kristo!
Azaliwa Kristo!
3. Usiku mtulivu!
Upendo mng’avu
Wang’ara mwako usoni
Na neema ya ukombozi,
Waja Bwana Mungu.
Waja Bwana Mungu.
Maandishi: Joseph Mohr, 1792–1848; Yametafsiriwa na John F. Young, 1820–1885
Muziki: Franz Gruber, 1787–1863
Luka 2:7–14