Muziki
Kwa Upole Twaimba


78

Kwa Upole Twaimba

Kwa unyenyekevu

1. Kwa upole twaimba,

Sabato yaja tena.

Tupumzike,

Tupumzike,

Na tushukuru Mungu

Baraka atupaye,

Baraka atupaye.

2. Ndiyo siku teule,

Mungu tumtafute,

Ni thawabu,

Ni thawabu,

Na tule sakramenti

Kumkumbuka Yesu,

Kumkumbuka Yesu.

3. Tuongeze sauti

Tuletapo zawadi

Ya upole,

Ya upole,

Kama dhabihu yetu

Ni kwa neema yake,

Ni kwa neema yake.

4. Ni mtukufu Kristo;

Ni zuri lake neno:

Fanya toba,

Fanya toba;

Japo dhambi nyekundu,

Msamaha atoa.

Msamaha atoa.

Maandishi: William W. Phelps, 1792–1872. Yalijumuishwa katika kitabu cha kwanza cha nyimbo za Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, 1835.

Muziki: Thomas C. Griggs, 1845–1903

Mafundisho na Maagano 59:8–12

Isaya 1:16–18