Muziki
Mwokozi Uvaaye Taji la Miiba


110

Mwokozi Uvaaye Taji la Miiba

Kwa kutafakari

1. Mwokozi uvaaye

Taji la miiba,

Mateso ubebaye,

Ya kebehi kubwa.

Wakuputa askari;

Wakunywesha nyongo;

Juu msalabani

Wateswa kwa kifo.

2. Hakuna mwenye dhambi

Aliye baniwa,

Utukufu kuhisi

Na kuokolewa.

Wa kusaliti wapo,

Wajua pendowe;

Nao wakuuao

Neema i bure.

3. Dhabihu ya ajabu

Imelipa deni;

Rehema yako ndefu

Ipo duniani.

Japo mwovu hudhuru,

Tu vitani bado,

Sasa hatuna hofu,

Twamwamini Kristo.

4. Sifa gani tutoe

Kushukuru, Bwana?

Msalabani pale

Juu ulifia,

Kwa mpango wa Mungu

Kuokoa nafsi.

Kwako mpendwa Yesu,

Twaleta hisani.

Maandishi: Karen Lynn Davidson, 1943–2019. © 1985 IRI

Muziki: Hans Leo Hassler, 1564–1612; umefanyiwa marekebisho na J. S. Bach, 1685–1750

2 Nefi 2:6–9

Mathayo 27:26–31, 34–35