155
Niwezeshe Kufundisha
Kwa hamasa
1. Niwezeshe kufundisha,
Bwana, unibariki.
Niweze kuwainua
Waongeze utii.
2. Nimfikie rafiki,
Aliye mpotevu.
Nimuongoze nuruni
Kwa Roho wako, Mungu.
3. Uelewa nipatie;
Nifanye mwangwi wako.
Niwe rafiki mpole;
Nijaze pendo lako.
4. Wapotevu kutafuta,
Na kuwaleta kwako.
Nifunze niwe mchunga;
Niwalishe kondoo.
Maandishi na muziki: Lorin F. Wheelwright, 1909–1987. ©1958, 1985 Lorin F. Wheelwright. Wimbo huu wa dini ni kwa matumizi ya kawaida ya kanisa, yasiyo ya kibiashara au matumizi ya nyumbani.
Mafundisho na Maagano 43:15–16
Yohana 21:15–17