167
Upendo ni Wake Bwana
Kwa utulivu
1. Upendo ni wake Bwana
Ahadi anatimiza,
Roho aziunganisha—
Jaza nafsi yangu;
Jaza nafsi yangu.
2. Upendo wa familia,
Unanileta kwa Bwana,
Upendo usioisha—
Jaza nafsi yangu;
Jaza nafsi yangu.
3. Upendo usioshindwa,
Unafanya mambo mema,
Utuletea uzima—
Jaza nafsi yangu;
Jaza nafsi yangu.
4. Ee Bwana nibadilishe
Niwe mwema kwa wengine,
Nilinde mwisho nifike—
Jaza nafsi yangu;
Jaza nafsi yangu.
Maandishi na muziki: Lorin F. Wheelwright, 1909–1987. © 1969, 1985 Lorin F. Wheelwright. Wimbo huu wa dini ni kwa matumizi ya kawaida ya kanisa, yasiyo ya kibiashara au matumizi ya nyumbani.
Yohana 17:20–23