Muziki
Msifu Aliye Juu


31

Msifu Aliye Juu

Kwa furaha

1. Msifu aliye juu,

Bwana Mungu Muumba,

Mwamba wa wokovu wetu,

Chanzo cha mamlaka.

Huniponya kwa upendo

Na kuituliza roho.

Sifa kwake milele!

2. Ayafanyayo kwa nguvu

Rehema yahifadhi.

Asubuhi na usiku

Jichowe halilali.

Katika ufalme wake,

Haki hutawala kote!

Sifa kwake milele!

3. Bwana yu karibu nasi,

Kwenye zote taabu,

Daima ndiye auni,

Amani na shauku.

Kama upendo wa mama,

Aongoza wake wana.

Sifa kwake milele!

4. Hivyo, katika taabu

Naimba sifa zako,

Ili wasikie watu

Nakuimbia wimbo.

Moyo, furahia Bwana,

Nawe nafsi, mwili pia!

Sifa kwake milele!

Maandishi: Johann J. Schütz, 1640–1690; yalitafsiriwa na Frances Elizabeth Cox, 1812–1897

Muziki: Kutoka Bohemian Brethren’s Songbook, 1566, umebadilishwa.

Zaburi 104:33

Zaburi 121:2–4