111
Kafufuka!
Kwa heshima
1. Kafufuka! Kafufuka!
Itangaze kwa shangwe.
Kifungo chake kavunja;
Watu wafurahie.
Kifo kina ukomo,
Ushindi ni wa Kristo.
2. Njoo na utakatifu;
Sifu ushindi wake.
Hakuna kiza cha wingu
Kuzuia miale,
Siku njema yaanza,
Ishara ya Pasaka.
3. Kafufuka! Kafufuka!
Amefungua mbingu.
Dhambi haitatufunga,
Tuna utakatifu.
Na nuru ya Pasaka
Machoni itang’aa.
Maandishi: Cecil Frances Alexander, 1818–1895
Muziki: Joachim Neander, 1650–1680
Marko 16:6–7