42
Kwa Wema wa Dunia
Kwa furaha
1. Kwa wema wa dunia,
Kwa uzuri wa mbingu,
Kwa pendo la daima
Lizungukalo kwetu.
[Chorus]
Bwana, Muumba wetu,
Twaimba kukusifu.
2. Kwa wema wa majira,
Mchana na usiku,
Bonde, mti na ua,
Anga na zake nuru.
[Chorus]
Bwana, Muumba wetu,
Twaimba kukusifu.
3. Kwa furaha, upendo,
Kaka, dada, wazazi,
Marafiki wajao,
Kwa mawazo mazuri.
[Chorus]
Bwana, Muumba wetu,
Twaimba kukusifu.
Maandishi: Folliott S. Pierpoint, 1835–1917
Muziki: Conrad Kocher, 1786–1872
Zaburi 95:1–6
Zaburi 33:1–6