Muziki
Kristo Mwokozi


66

Kristo Mwokozi

Kwa hamasa

1. Kristo Mwokozi ni Mfalme!

Naimba kwa moyo wote;

Kwa furaha nitasifu,

Niseme amina kuu.

Kristo Mwokozi; ndiye Neno.

Aliishi kati yao,

Alifanya miujiza

Tulisifu lake jina.

2. Kristo Mwokozi; ndiye Bwana!

Alikuja kutawala

Kati yao, wanadamu,

Na dhambi awanusuru.

Kristo Mwokozi; ndiye nija.

Karithi yote ya Baba,

Asema: “Njooni kwangu,

Na ninyi muwe na Mungu.”

3. Kristo Mwokozi — Bwana, Mungu!

Neno lake lina nguvu.

Nitamwabudu kwa dhati;

Ndiye chanzo cha ukweli.

Kristo Mwokozi ni dhamana.

Kwa Shetani hunitoa.

Nitaishi kwa upendo

Kule mbinguni alipo.

4. Kristo Mwokozi ni Muumba!

Kwake ndoto natimiza;

Nipitapo kwenye dhiki,

Ye husema: “Utastawi.”

Kristo Mwokozi niwe naye

Siku hiyo, kwa vyovyote,

Akija kwa walimwengu

Kutawala kati yetu.

Maandishi: Bruce R. McConkie, 1915–1985. © 1972 IRI

Muziki: John Longhurst, kuz. 1940. © 1985 IRI

2 Nefi 25:23, 26, 29

Mormoni 7:5–7