Muziki
Enyi Wana wa Bwana


26

Enyi Wana wa Bwana

Kwa kushangilia

1. Enyi wana wa Bwana,

Tuimbe kwa umoja.

Tupaze wetu wimbo

Kwake atawalapo.

Tutasafishwa wote,

Na makosa yafutwe,

Tutapoacha dhambi,

Tuishi kwa amani.

2. Tutakavyofurahi

Tumwonapo Mwokozi!

Aja kwa utukufu,

Kukomesha maovu.

Nyimbo tutamwimbia

Mfalme wetu, Bwana.

Tutajaa upendo,

Woga kufika mwisho!

3. Tutakuwa wasafi,

Tutaishi nuruni.

Tutamwimbia sifa;

Shangwe tutazipaza.

Dunia isafishwe

Viumbe vyake vyote,

Viishi kwa upendo;

Furaha kila moyo.

Maandishi: James H. Wallis, 1861–1940

Muziki: Lahani ya Uhispania; umepangiliwa na Benjamin Carr, 1768–1831

Mafundisho na Maagano 133:25, 33, 56

Ufunuo 7:9–17