118
Ukaja Usiku Ule
Kwa uchangamfu
1. Ukaja usiku ule,
Wimbo wa zamani,
Wakiimba malaika
Kwa kupiga vinubi.
“Amani ulimwenguni
Yatoka kwa Bwana.”
Dunia iwe tulivu
Kuwasikiliza.
2. Bado waja na mawingu
Kwa mbawa tulivu,
Na muziki unavuma
Katika ulimwengu.
Nyikani penye huzuni
Wajiinamia,
Juu ya kelele nyingi
Wanawaimbia.
3. Manabii walijua
Siku zitakuja.
Na miaka ipitapo
Yote yatatokea,
Ndipo vitakiri vyote
Bwana wa Amani.
Nayo dunia iimbe
Na wote mbinguni.
Maandishi: Edmund H. Sears, 1810–1876
Muziki: Richard S. Willis, 1819–1900
Luka 2:8–17