Muziki
Nachungwa na Bwana


54

Nachungwa na Bwana

Kwa utulivu

1. Nachungwa na Bwana; sikosi kitu.

Nalishwa pazuri; nina amani.

Naongozwa penye maji tulivu,

Kwake sipotei na sinyanyaswi,

Kwake sipotei na sinyanyaswi.

2. Nipoteapo kwenye bonde la kifo,

U Mlezi wangu, sihofu mwovu.

Nitaimarishwa na fimbo yako.

Sidhuriki kama upo karibu.

Sidhuriki kama upo karibu.

3. Nipatwapo na dhiki, nina chakula.

Kikombe chajaa baraka tele.

Wanipaka kichwa changu mafuta.

Nini zaidi ya hayo niombe?

Nini zaidi ya hayo niombe?

Maandishi: James Montgomery, 1771–1854; kutokana na Zaburi 23

Muziki: Thomas Koschat, 1845–1914

Zaburi 23

Isaya 26:3–4