70
Tubarikie Mfungo
Kwa hamasa
1. Bwana tunakusujudu,
Mbele zako twaja,
Tunaomba kwa sauti—
Je, utaongea?
[Chorus]
Tubarikie mfungo
Na nafsi ulishe,
Ili ukawe na sisi
Tufurahi nawe.
2. Tumelisha wahitaji,
Maskini twawapa,
Tukawalaki wageni—
Je, utaongeza?
[Chorus]
Tubarikie mfungo
Na nafsi ulishe,
Ili ukawe na sisi
Tufurahi nawe.
3. Kama mashahidi twaja
Kukupa shukrani,
Kwa kutenda miujiza,
Bwana tubariki.
[Chorus]
Tubarikie mfungo
Na nafsi ulishe,
Ili ukawe na sisi
Tufurahi nawe.
Maandishi: John Sears Tanner, kuz. 1950. © 1985 IRI
Muziki: James B. Welch, kuz. 1950. © 1985 IRI
Isaya 58:6–11