Muziki
Sifa kwa Aliyenena na Bwana


17

Sifa kwa Aliyenena na Bwana

Kwa shauku

1. Sifa kwa aliyenena na Bwana!

Nabii huyo alitawazwa.

Alifungua kipindi cha mwisho,

Watamheshimu mataifa.

[Chorus]

Shangwe kwa nabii kwenda mbinguni!

Waasi sasa, bure wapinga.

Akichangamana nao Miungu;

Na kifo hakimshindi tena.

2. Atakumbukwa kwa kufia dini;

Jina lake litaheshimiwa!

Damu waliyoimwaga waovu,

Kwake Mungu itamtetea.

[Chorus]

Shangwe kwa nabii kwenda mbinguni!

Waasi sasa, bure wapinga.

Akichangamana nao Miungu;

Na kifo hakimshindi tena.

3. Hauna mwisho ukuhani wake.

Milele funguo amiliki.

Ataingia katika ufalme,

Kutuzwa kati ya manabii.

[Chorus]

Shangwe kwa nabii kwenda mbinguni!

Waasi sasa, bure wapinga.

Akichangamana nao Miungu;

Na kifo hakimshindi tena.

4. Dhabihu yatuletea baraka.

Kote maovu yatajutiwa.

Zindukeni tupiganie haki.

Jina la Joseph litakumbukwa.

[Chorus]

Shangwe kwa nabii kwenda mbinguni!

Waasi sasa, bure wapinga.

Akichangamana nao Miungu;

Na kifo hakimshindi tena.

Maandishi: William W. Phelps, 1792–1872

Muziki: Wimbo wenye asili ya Uskoti

Mafundisho na Maagano 135

2 Nefi 3:14–15