81
Kama Umande Wa Mbingu
Kwa dhati
1. Kama umande wa mbingu
Ushukavyo nyasini
Ili kuzitia nguvu
Pamoja na ulinzi,
2. Hivyo mafundisho, Bwana,
Yashuke toka kwako,
Yaweze kutosheleza
Kaziyo ya upendo.
3. Ona waumini, Bwana;
Timizia ahadi.
Kutoka mbinguni tuma
Umande wa uhai.
4. Sikia maombi yetu.
Mtume Roho aje,
Ili watu wasujudu
Pia wakutukuze.
Maandishi: Thomas Kelly, 1769–1854
Muziki: Joseph J. Daynes, 1851–1920
Kumbukumbu la Torati 32:2
Isaya 55:10–11