91
Mungu Baba Twaomba
Kwa unyenyekevu
1. Mungu Baba twaomba;
Tutumie neema.
Tukila sakramenti,
Twalindwa na Mwokozi.
2. Tupe neema yako
Na tabasamu lako.
Na mkate tukila,
Thibitisho twaomba.
3. Na tukiyanywa maji,
Roho awepo nasi.
Tusamehe, Ee Bwana,
Bariki tuwe wema.
Maandishi: Annie Pinnock Malin, 1863–1935
Muziki: Lous M. Gottschalk, 1829–1869; umefanyiwa marekebisho na Edwin P. Parker, 1836–1925