161
Twalipenda Neno Lako
Kwa hamasa
1. Twalipenda neno lako
Likihubiriwa.
Hutuinua mioyo
Ili kutukuza.
2. Twapenda kusoma neno
Kwa wazo na sala.
Anatuongoza Roho;
Twahisi kulindwa.
3. Twapenda kuitangaza
Injili ya Kristo.
Twapeana ushuhuda
Wa wokovu wako.
4. Twakushukuru kwa neno;
Kwa nyimbo twasifu.
Tupe uelewa, Kristo,
Tuwe watiifu.
Maandishi: Marvin K. Gardner, kuz. 1952. © 1985 IRI
Muziki: Robert Cundick, 1926–2016. © 1985 IRI