Muziki
Zashuhudia Mungu


39

Zashuhudia Mungu

Kwa upole

1. Ardhi na yake maua,

Mvua, nuru za anga,

Pande zote mbinguni,

Fahari ya bahari—

Kote chini na juu

Vyashuhudia Mungu.

2. Mabonde, nayo milima,

Vijito asilia,

Ndege, hata upepo,

Kwa sauti nyororo —

Nyimbo zao tukufu,

Zashuhudia Mungu.

3. Zianzapo tumaini

Kutujaa moyoni,

Raha nayo ijapo

Nyumbani tuishipo,

Sauti zote juu

Zashuhudia Mungu.

Maandishi: Thomas R. Taylor, 1807–1835, yamebadilishwa. Yalijumuishwa katika kitabu cha kwanza cha nyimbo za Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, 1835.

Muziki: Thomas C. Griggs, 1845–1903

1 Yohana 4:7–8

Musa 6:63