105
Kwa Ukumbusho wa Kristo
Kwa sala
1. Kwa ukumbusho wa Kristo,
Baba yetu twakutana.
Tunaomba Roho wako,
Mlioyo yetu kuponya.
2. Bwana, kule Gethsemane
Kikombe hakukiacha.
Kwa ajili yetu wote
Msalaba alibeba.
3. Kwa mwili na damu yake,
Deni la dhambi kalipa.
Tuapokea kikombe,
Na mkate kwa heshima.
4. Sakramenti hii, Baba,
Takasa kwa kila nafsi.
Yule anayepokea,
Akaishi kwa usafi.
Maandishi: Frank I. Kooyman, 1880–1963. © 1948 IRI
Muziki: Alexander Schreiner, 1901–1987. © 1948 IRI