14
Nabii Mpendwa
Kwa hamasa
1. Nabii mpendwa, twamuomba
Akupe faraja, Mungu Baba.
Miaka ijavyo na uzee,
Na mwangaza wako uangaze,
Na mwangaza wako uangaze.
2. Tunakuombea mioyoni,
Ukapewe nguvu na Mwokozi
Ya kutuongoza kila siku,
Ya kuiangaza njia yetu,
Ya kuiangaza njia yetu.
3. Tunakuombea, twakupenda,
Na maombi yetu yasikika.
Ubarikiwe na Mungu wetu,
Na akupatie kila kitu,
Na akupatie kila kitu.
Maandishi: Evan Stephens, 1854–1930
Muziki: H. A. Tuckett, 1852–1918; umefanyiwa marekebisho na Evan Stephens, 1854–1930