Muziki
Kazi Tamu


79

Kazi Tamu

Kwa hamasa

1. Kazi tamu, Mungu wangu,

Jina lako kulisifu,

Pendo lako kuonyesha,

Ukweli wako kusema.

2. Siku tamu ya Sabato,

Ya dunia niachapo.

Nitaimba kwa uzuri

Kwa kinubi cha Daudi!

3. Moyo wangu utasifu

Kazi yako kushukuru.

Neema yako yang’ara!

Wosia wako, hekima!

4. Ni ushindi ulioje

Kwa jina lako milele,

Kwa furaha nikiona

Uso wako uking’aa!

5. Sitasumbuliwa kamwe

Na dhambi, adui yule,

Maadui watashindwa,

Shetani hatasumbua.

6. Na kisha nitayapata

Yote niliyoyataka,

Nitafanya kila kitu

Milele mbinguni juu.

Maandishi: Isaac Watts, 1674–1748

Muziki: John J. McClellan, 1874–1925

Zaburi 92:1–5

Enoshi 1:27