Muziki
Tuishangilie Siku ya Wokovu


3

Tuishangilie Siku ya Wokovu

Kwa uchangamfu

1. Tuishangilie siku ya wokovu,

Sisi sio wageni duniani.

Habari njema, mataifa na watu,

Wokovu waja hivi karibuni.

Ahadi kwa Wema zitapotimizwa,

Nao hawatasumbuliwa tena,

Kama Edeni, dunia itakuwa,

Yesu atasema, “Njoo nyumbani.”

2. Sote tutapendana bila ghadhabu,

Tutaungana na kuacha dhambi.

Na wakati wakiogopa waovu,

Tutangojea siku ya Mwokozi.

Ahadi kwa Wema zitapotimizwa,

Nao hawatasumbuliwa tena,

Kama Edeni, dunia itakuwa

Yesu atasema, “Njoo nyumbani.”

3. Tutaamini mkono wa Yehova

Kutuongoza nyakati za mwisho.

Uangamizaji utakapoisha,

Tutafufuka Mfalme ajapo.

Ahadi kwa Wema zitapotimizwa,

Watatunukiwa na malaika,

Kama Edeni, dunia itakuwa,

Na Wema wataungana na Kristo.

Maandishi: William W. Phelps, 1792–1872. Yalijumuishwa katika kitabu cha kwanza cha nyimbo za Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, 1835.

Muziki: Henry Tucker, 1826–1882

Musa 7:61–67

Makala ya Imani 1:10