Muziki
Mungu, Msaada Wetu


171

Mungu, Msaada Wetu

Kwa heshima

1. Mungu, msaada wetu,

Tumamini ndiwe.

Wewe ni hifadhi yetu,

Na kwetu milele.

2. Na katika kiti chako,

Twaweza kupona.

Yatosha mikono yako,

Kwani yatulinda.

3. Kabla kupangwa vilima,

Hata ulimwengu,

Enzi na enzi daima,

Utabaki Mungu.

4. Mungu, msaada wetu

Tumaini ndiwe.

Kuwa nuru yetu kuu

Na kwetu milele.

Maandishi: Isaac Watts, 1674–1748. Yalijumuishwa katika kitabu cha kwanza cha nyimbo zaKanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, 1835.

Muziki: William Croft, 1677–1727

Zaburi 90:1–2

Zaburi 91:1–2

Zaburi 48:14